post-feature-image
HomeHABARI

Dhamana ya Lissu kujulikana leo

  Thursday, July 27, 2017   Dar es Salaam. Hatima ya dhamana ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inatarajiwa kujuli...


Dar es Salaam. Hatima ya dhamana ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu inatarajiwa kujulikana leo, Julai 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Uamuzi wa kumpa dhamana au la utatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Julai 24 jopo la mawakili wanne wa Serikali, Kishenyi Mutalemwa, Simon Wankyo, Paul Kadushi na Tulumanywa Majigo waliwasilisha hoja mahakamani hapo wakiomba Lissu anyimwe dhamana.

Jopo la mawakili 18 wanaomtetea Lissu, likiongozwa na Fatma Karume na Peter   Kibatala liliomba mteja wao apewe dhamana.

Lissu alipelekwa katika Gereza la Segerea na leo hatima ya dhamana yake itajulikana.

Katika shauri linalomkabili, Lissu anadaiwa Julai 17 eneo la Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam alitoa maneno  ya uchochezi kuwa, 'Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ni ya kibaguzi wa kifamilia, kikabila, kikanda na kidini.'

Anadaiwa kusema vibali vya kazi (working permit) vinatolewa kwa wamishenari wa Kikatoliki tu, huku madhehebu mengine yakielezwa kupanga foleni uhamiaji.

Pia, anadaiwa kusema viongozi wakuu wa Serikali wanachaguliwa kutoka kwenye familia, kabila na ukanda… Acheni woga pazeni sauti… Kila mmoja wetu... Tukawaambie wanaompa msaada  wa pesa, Magufuli na Serikali yake  kama tulivyowaambia  wakati wa Serikali ya makaburu, hii Serikali isusiwe na jumuiya ya kimataifa, isusiwe kisiasa, kiuchumi na kidiplomasia  kwa sababu ya utawala huu wa kibaguzi… yeye ni dikteta uchwara.

Wakili wa Serikali, Kishenyi alidai maneno hayo yalikuwa na lengo la  kuleta chuki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kusomewa shtaka, Hakimu Mashauri alimtaka Lissu aeleze kama analikubali shtaka hilo au analikataa.

Lissu alieleza kuwa, “kusema ukweli haijawahi kuwa kosa la jinai kwa hiyo si kweli.”
Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Dhamana ya Lissu kujulikana leo
Dhamana ya Lissu kujulikana leo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMkcW0EifLoCwYTAjSH3k2WHvAas7AO85AQNrKPiMO17MnTPe4JpHyT7DN9nrb7xA3EAtleW3o3twxibhQqztAcnIe3wha4rGl5R1r8oMJK5ljd4klXo8WyHeP1ugaJ53919X1EkkoEDI/s400/DFhRQnqXgAAILHJ.jpg.pagespeed.ce.Onnvkw-DBB.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhMkcW0EifLoCwYTAjSH3k2WHvAas7AO85AQNrKPiMO17MnTPe4JpHyT7DN9nrb7xA3EAtleW3o3twxibhQqztAcnIe3wha4rGl5R1r8oMJK5ljd4klXo8WyHeP1ugaJ53919X1EkkoEDI/s72-c/DFhRQnqXgAAILHJ.jpg.pagespeed.ce.Onnvkw-DBB.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/dhamana-ya-lissu-kujulikana-leo.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/dhamana-ya-lissu-kujulikana-leo.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago