post-feature-image
HomeHABARI

Polisi Akatwa Mkono Katika Ugomvi wa Kugombea Mwanamke

18JULY2017 Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarim...

Friday, April 20, 2018 Polisi waua majambazi wanne Pwani
Rais Magufuli achukizwa na Mitandao ya Kijamii
BREAKING NEWS: Masogange amefariki dunia

Jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Tarime-Rorya, linawashikilia watu wawili wakazi wa Mtaa wa Nkende mjini Tarime wakidaiwa kumkata mkono Mkaguzi wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana-River cha nchini Kenya, James Mnuve (50), wakati wakimgombania mwanamke.

Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, SACP Henry Mwaibambe, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kukatwa mkono Mkaguzi huyo wa Polisi wa nchini Kenya. 

Mwaibambe alidai kuwa tukio hilo lilitokea Julai 13 mchana katika mtaa wa Nkende mjini Tarime ambapo vijana hao walitenda kosa hilo. 

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Michael Omahe, anayedaiwa kumtorosha mwanamke huyo, Anne Njeri, kutoka Kenya na kumleta Tanzania kisha kuishi naye kinyumba huku akisaidiana na rafiki yake, Daniel Onchiri.

“Mwanamke huyo (Njeri) anadaiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi pia na askari James Mnuve na walikuwa wakiishi huko Tana River nchini Kenya, baada ya kuondoka, Julai 13 mchana askari huyo alimfuatilia kutoka Kenya hadi Mtaa wa Nkende, Tarime alipokuwa anaishi na kijana aliyemtorosha (Michael Omahe),” alisema Kamanda.

Akaongeza, “Alipofika Mtaa wa Nkende alimkuta Michael, pamoja na rafiki yake huyo wakiwa na mwanamke huyo na hapo ndipo ugomvi ulipoanza kwani askari James alitaka kuondoka na mwanamke huyo na zikazuka vurugu kubwa na kusababisha Mnuve kukatwa kwa kutumia panga.”

Aidha Kamanada huyo alisema kuwa, “Jeshi la Polisi tulifika kwenye eneo la tukio mapema na kuweza kuwakamata watuhumiwa wote watatu; Marandi, Ochiri na mwanamke huyo na kisha tukawahoji kabla ya kuwafikisha mahakamani huku majeruhi akiwa amepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa matibabu.” 

Majeruhi James anadai kuwa yeye ni Inspekta wa Polisi wa Kituo cha Ngamba Tana River nchini Kenya na mwanamke huyo, Njeri Wanjoi, ni mke wake.
Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Polisi Akatwa Mkono Katika Ugomvi wa Kugombea Mwanamke
Polisi Akatwa Mkono Katika Ugomvi wa Kugombea Mwanamke
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvoyDI0gg2UXfZb4yJJJqyxSCt4kc_IvR0s0xYwQZSM2DafCvElxDb1oh2JW48nwog_npmn_I21uur_-2NzDyS-KfzHWRZfnqwtT_t29W-nO_bJuabynY6B21iRvOWKBsBbi4MKFibqvCR/s1600/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvoyDI0gg2UXfZb4yJJJqyxSCt4kc_IvR0s0xYwQZSM2DafCvElxDb1oh2JW48nwog_npmn_I21uur_-2NzDyS-KfzHWRZfnqwtT_t29W-nO_bJuabynY6B21iRvOWKBsBbi4MKFibqvCR/s72-c/1.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/polisi-akatwa-mkono-katika-ugomvi-wa.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/polisi-akatwa-mkono-katika-ugomvi-wa.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago