Archive Pages Design$type=blogging

Mambo 6 yakuzingatia katika ndoa.

6 AUGUST  2017   1. kucheka pamoja Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na h...

1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au  dhambi?

Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.

4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.

Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.

COMMENTS

Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Mambo 6 yakuzingatia katika ndoa.
Mambo 6 yakuzingatia katika ndoa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikXrYXjZqaE_KCihf1xtpGKqyYwS18fCrfnX0yVx1ALcHI1ygVPr9KcLN7_9fzyDbBnDBuH6Otq_6SFX4qA9z06kqEE4BzhfowNPK527rh8AEKgZN9NJjSpZ8ZVVlFFHax8pMxBvZV2FDM/s640/black-couple-casually-talking-each-footage-023901615_prevstill.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEikXrYXjZqaE_KCihf1xtpGKqyYwS18fCrfnX0yVx1ALcHI1ygVPr9KcLN7_9fzyDbBnDBuH6Otq_6SFX4qA9z06kqEE4BzhfowNPK527rh8AEKgZN9NJjSpZ8ZVVlFFHax8pMxBvZV2FDM/s72-c/black-couple-casually-talking-each-footage-023901615_prevstill.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/08/mambo-6-yakuzingatia-katika-ndoa.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/08/mambo-6-yakuzingatia-katika-ndoa.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago