Siku ya leo naomba tujifunze elimu mpya kabisa ya uzazi ambapo mwanamke yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kam...
Siku
ya leo naomba tujifunze elimu mpya kabisa ya uzazi ambapo mwanamke
yeyote anaweza kupata ujauzito wenye watoto mapacha hata kama si asili
ya ukoo wake, ambavyo wengi wanavyosema.
Nimetumia
neno ‘mwanamke yeyote’ kwa sababu kuna imani ya miaka na miaka kwamba,
si kila mwanamke anaweza kupata ujauzito bali itategemea na asili yake.
Imani ya kale kuhusu ujauzito
Baadhi
ya mila na desturi, hasa katika nchi za Kiafrika zinaamini kwamba,
mwanamke kupata watoto mapacha kunatokana na urithi wa kizazi chake,
kuanzia mababu wa upande mmoja kati ya wanandoa hivyo uzao huo hufuata
mkondo kwa miaka na miaka.
Wengi
wakipata mapacha huulizwa kama kwenye kizazi chake, kuna watoto
mapacha. Akitokea mama akasema hakuna, basi huaminika kwamba lazima
upande wa mwanaume kuna waliowahi kuzaliwa mapacha hata kama si katika
miaka ya karibuni.
Imani
hii ni ya kizamani sana, ukweli ni kwamba mwanamke yeyote mwenye sifa
ya kushika mimba na kuzaa, anaweza kupata ujauzito na kuzaa mapacha bila
kujali asili ya kizazi chake.
Kwa
nchi zilizoendelea wanawake wanaweza kuzaa mapacha kwa kupandikiza
mayai yaliyopevuka kwa kutegemea na idadi unayoitaka mwenyewe lakini
bila kujua wangeweza kuzaa hata bila ya kupandikizwa.
Nina
ushahidi kuwa, baadhi ya wanawake huenda kwa waganga wa kienyeji kwa
lengo la kupatiwa dawa ya kuwasaidia kuzaa mapacha, jambo ambalo si
sahihi na halipo. Sanasana utaliwa pesa zako bure na mapacha usiwapate.
Wanawake
wengi wanaoongoza kwa kushika mimba za mapacha ni wale ambao wakati wa
kulala wanabadili staili mara kwa mara. Mara nyingi inashauriwa kuwa,
mwanamke akishaingia kwenye siku zake za hatari kulingana na mzunguko
wake wa hedhi, akutane kimwili na mumewe au mwanaume anayetaka kuzaa
naye.
Baada
ya tendo la ndoa, mwanaume anashauriwa kulala kwa kujigeuzageuza
kitandani. Hapa namaanisha kwamba, akiwa amelala, ajigeuze kuangalia
juu, kulalia ubavu wa kulia, kushoto, kulala kifudifudi kwa usiku kucha.
Fanya
hivi kwa kurudiarudia siku kadhaa katika kipindi hicho cha hatari, hapo
uwezekano wa kushika mimba ya mapacha utakuwa mkubwa sana.