Archive Pages Design$type=blogging

Chuo Cha Muslim Morogoro chatoa fursa kwa Watanzania kusoma Lugha ya Kichina

, July 26, 2017   MAONESHO  ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yamefunguliwa rasmi leo na Waziri M...

MAONESHO ya Elimu ya Juu yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja yamefunguliwa rasmi leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Kassim Majaliwa Kassim huku yameonesha mwitikio mzuri kwa vyuo mbalimbali vilivyojitokeza kudahili wanafunzi wanaotaka kujiunga na kozi  tofauti kwenye vyuo vyao.

Ili kutoa fursa ya elimu kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo, Chuo cha Muslim Morogoro kimewataka wanafunzi wachangamkie fursa ya elimu ya lugha ya Kichina inayopatikana katika chuo chao kwani kimeweza kuwasaidia wanafunzi wengine kufahamu lugha hiyo pamoja na kupata nafasi za kusoma nchini China bure.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Afisa Habari wa Chuo cha Muslim Morogoro Ngaja Mussa amesema kuwa wanatoa kozi ya elimu hiyo ya lugha ya kichina kwa wanafunzi wote wanaotaka kuifahamu na pia utakaposoma kwa mwaka mmoja na kuifahamu vizuri lugha hiyo unapata nafasi ya kusoma nchini China.

Ngaja amesema kwa sasa kuna walimu takribani saba wanatoa mafunzo ya elimu hiyo katika chuo chao, mbali na kozi hiyo ya lugha ya Kichina wanatoa pia kozi mbalimbali katika ngazi ya astashahada, stashahada na shahada.

Kwa ngazi ya shahada kwa mwaka 2017/18  wana kozi za Bachelor of Arts with Education pamoja na Bachelor of law with Shariah huku ngazi ya Astashahada na Stashahada wana kozi za  Procurement and Logistics Management, Journalism, Medical Labaratory Technology, Science and Laboratory Technology, Laws with Shariah pamoja na Islamic Bankinga and Finance
.

COMMENTS

Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Chuo Cha Muslim Morogoro chatoa fursa kwa Watanzania kusoma Lugha ya Kichina
Chuo Cha Muslim Morogoro chatoa fursa kwa Watanzania kusoma Lugha ya Kichina
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMV19pLx4a9YOMV27Kk2aBOz14OZf4SIS3JOhskildkiu4RLDF6D7MkPNLdgu1MfkNMj_wzuWR80YU0F-8BBP_yh_mtaQON6cAmvAWIMeJa4G9T1pE0xjGjG7iHrJU7FX7LL0RUAB7Dfo/s400/DSCF3780+-+Copy+-+Copy.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMV19pLx4a9YOMV27Kk2aBOz14OZf4SIS3JOhskildkiu4RLDF6D7MkPNLdgu1MfkNMj_wzuWR80YU0F-8BBP_yh_mtaQON6cAmvAWIMeJa4G9T1pE0xjGjG7iHrJU7FX7LL0RUAB7Dfo/s72-c/DSCF3780+-+Copy+-+Copy.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/chuo-cha-muslim-morogoro-chatoa-fursa.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/chuo-cha-muslim-morogoro-chatoa-fursa.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago