post-feature-image
HomeMAKALA

Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio

july  26, 2017   Pesa hii ina majina mengi hii ni kutokana na mahali husika wapo wanaita pesa ni sadaka, nauli, zaka, fungu la...

Vitu unavyotakiwa kujua kabla ya kuoa / kuolewa
Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi
Mambo 10 ambayo ni Sumu katika Mapenzi


Vilevile kuna wakati mwingine Katika maisha yetu ya kila siku tunasema pesa ndo kila kitu. Ni kweli kabisa juu ya msemo huo lakini kuwa na pesa bila mawazo  chanya ni bure, hii ni sawa na kuzima moto kwa chafya. Unashangaa huo ndo ukweli watu wengi tunapata pesa lakini hatujui tuitumie vipi pesa hiyo ili iweze kujisalisha. zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha matumizi mabaya ya fedha.
Leo katika makala haya nitakwenda kukuelezea juu ya matumizi mabaya ya pesa yanayofanya kila siku tuwe katika hali ya umaskini.

Yafuatayo ndiyo matumizi mabaya ya pesa.

1. Kutokuwa na mpangilio wa matumizi ya pesa.
Moja ya changamoto kubwa inayowakumba wengi wetu ni kwamba hatuana mapangalio sahihi juu ya matumizi ya fedha. Tupo baadhi yetu ambao hutamani kila kitu ambacho tunakiona mbele yetu na kukinunua hata kama kitu hicho hakikuwepo katika mapango wa kukinunua. Tupo baadhi yetu tukiwa tunatembea hasa pale tunapokuwa na pesa tukiona hiki na kile ni lazima tununue hiyo siyo nidhamu ya fedha. kufanya hivi ni kujitengenezea kaburi la umaskini wewe mwenyewe.

Pia kuna baadhi ya watu wakipata mishara utajua tu kwa kuona matumizi yao wanayoyafanya. Kufanya hivo ni Kujirudisha nyuma mwenyewe jambo lamsingi la kufanya juu ya matumizi sahihi ni kuwa na mapagalio mzuri wa pesa nunua kitu ambacho umepanga kununua. Pia Hakikisha ya kwamba kila pesa unayoipata na kuitumia Unaiandika katika daftari lako la kumbumbuka hii itakusaidia kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha maana utakuwa unajua kila faida na hasara ya jambo unalolifanya.

2. Kukopa pesa hovyo
Hili ndilo kosa kubwa ambao linawaelemea watu wengi sana. Nadhani utakuwa shaidi mzuri ni jinsi gani!  madeni yanavowatesa watu au yanavyokutesa wewe. Wapo baadhi ya watu wanakopa pesa katika taasisi za kifedha lakini hawana elimu ya kutosha juu ya mikopo hiyo hasa katika kuangalia mkopo utakuwa na faida au hasara. Wengi Hawaelewi kuhusiana na mkopo hasa swala zima la kulipa riba. Wao hutazama mkopo kama seheme ya kutatua changamoto zao tu.

Utashangaa kwa mfano mtu anakopa shilingi laki tisa na anatakiwa kurudisha milioni moja ndani ya mwezi mmoja.  Kwa kuwa pesa hiyo haukujua juu ya riba hiyo pindi unaposhindwa kuirejesha utajikutana unanguna na wale wanaosema mkopo ni hauna faida yeyote.

Maana yangu ni kwamba kukopa sio kubaya ila jaribu kupata elimu ya kutosha juu ya mikopo, na jaribu kufanya uchunguzi wa mkopo hasa swala la riba. Jaribu kufanya mlinganisho kutoka taasisi moja na nyingine juu ya mkopo hasusani swala la riba kufanya hivi  itakusaidia kujua ni mkopo gani unakufaa na utaweza kuurejesha bila matatizo yeyote.

Tukiachana maswala ya mikopo katika mataasisi ya kifedha wapo baadhi ya watu ni wakopaji wazuri kwa watu wengine kama vile nguo, viatu na pesa. Usiwe na madeni ambayo yamezidi kwa kiwango kikubwa kwani kuwa na madeni kwa kiasi kikubwa yanakurudisha nyuma kwa namna moja au nyingine.chanzo muungwana.
Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio
Matumizi Mabaya Ya Fedha Ni Adui Wa Mafanikio
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2Po8hBxcEFjNf7JccxO8NFow8kH1zuH7LL-M-QTzkdzE1SV_7Z2zhfXG-l3GV5eX7DdFPd39COxnbPBSn521bpIZ1IU72yT6Cu565h04_9E52JptzLS2JAxvufeXGuMc8WkouG7N__nIi/s400/pesa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj2Po8hBxcEFjNf7JccxO8NFow8kH1zuH7LL-M-QTzkdzE1SV_7Z2zhfXG-l3GV5eX7DdFPd39COxnbPBSn521bpIZ1IU72yT6Cu565h04_9E52JptzLS2JAxvufeXGuMc8WkouG7N__nIi/s72-c/pesa.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/matumizi-mabaya-ya-fedha-ni-adui-wa.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/matumizi-mabaya-ya-fedha-ni-adui-wa.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago