Archive Pages Design$type=blogging

Trump atoa ishara za kubadili msimamo kuhusu tabia nchi july14 Hivi ni viunganisho vya nje na vitafungua katika dirisha mpya Sambaza...

Trump atoa ishara za kubadili msimamo kuhusu tabia nchi

july14
Trump atoa ishara za kubadili msimama kuhusu tabia nchi Ufaransa
Image captionTrump atoa ishara za kubadili msimamo kuhusu tabia nchi Ufaransa
Rais wa Ufaransa Manuel Macron amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa rais Trump kujitoa katika makubaliano ya tabia nchi ya Paris na kwamba Ufaransa itaendelea na juhudi zake kuhusu makubaliano hayo.
''Kuhusu tabia nchi tunajua tofauti yetu'', Bwana Macron alisema mjini Paris siku ya Alhamisi , akiongezea: Ni muhimu kusonga mbele.
Akizungumza pamoja na Macron, rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba huenda Marekani ikabadili msimamo wake lakini hakutoa maelezo ya zaidi.
''Kitu kitafanyika kwa heshima ya makubaliano ya Paris''.
Bwana Trump aliongezea: Tutaona kile kitakachofanyika.
Rais huyo wa Marekani alijiondoa katika makubaliano hayo 2015 mwezi uliopita, akitaka kujadili upya kwa makubaliano hayo ili kutoiweka Marekani katika hatua isiyo na manufaa kwake kibiashara.
Bwana Macron alisema kuwa ni muhimu kuweka makubaliano hayo kando huku viongozi hao wawili wakizungumza vile watakavyofanya kazi kuhusu maswala kama vile kusitishwa kwa mapigano nchini Syria na ushirikiano wa kibiashara.
Tuna tofauti zetu; Bwana Trump ana ahadi za uchaguzi alizowapatia raia wa tafa lake na pia mimi nilikuwa na ahadi, je vitu hivi vinapaswa kuturudisha nyuma katika maswala yote? Hapana, alisema Macron.
Bwana Macron na Trump baadaye walizungumza kuhusu juhudi za pamoja za mataifa hayo katika kukabiliana na ugaidi na hususan kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria na Iraq.
"Marekani inahusishwa pakubwa katika vita vinavyoendelea nchini Iraq'', alisema Macron, ''ningependa kumshukuru rais kwa kila kitu kinachofanywa na wanajeshi wa Marekani katika eneo hili''.
''Tumekubaliana tuendeleze na juhudi zetu za pamoja'' ,aliongezea ''husuasan mipango baada ya vita''.
Bwana Macron alisema kuwa Ufaransa itaweka mikakati kadhaa ili kusaidia kuimarisha uthabiti katika eneo hilo.
chanzo:bbc

COMMENTS

Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ
https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/59BC/production/_96927922_trumpandmacron.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/trump-atoa-ishara-za-kubadili-msimamo.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/trump-atoa-ishara-za-kubadili-msimamo.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago