Archive Pages Design$type=blogging

Watumishi wa umma sasa kupokea mishahara pamoja

Tuesday, July 18, 2017     Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki   Dar e...

 




Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki 

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki, amesema katika mwaka huu mpya wa fedha watumishi wa umma watakuwa wanalipwa mishahara kwa wakati mmoja ili kupunguza matatizo ya mishahara yanayojitokeza.
Kairuki ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Julai 18 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya mpya ya Ubungo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza jana katika halmashauri hiyo.
Amesema awali watumishi hao walikuwa wanapata mishahara yao kwa nyakati tofauti lakini sasa wataingizia mishahara yao moja kwa moja katika akaunti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) badala ya kupitia benki za biashara.
"Hatutaki itokee huyu amewekewa mshahara tarehe 27, huku mwingine akienda kuangalia salio katika akaunti anaambiwa bado lakini sasa hivi itakuwa wakati mmoja," amesema Kairuki huku akishangaliwa na watumishi wa halmashauri hiyo.
Alisisitiza lengo la kuweka mfumo huo ni kuhakikisha watumishi wote wanapata mshahara wao wakati mmoja na hiyo itasaidia Serikali kusimamia kwa umakini mishahara.
Amefafanua kwamba siku tatu kabla mshahara haujaingizwa katika akaunti ya mtumishi, mwajiri sekta husika atapelekewa orodha ya watumishi watakaotakiwa kulipwa mishahara.
"Matumaini yangu waajiri watakuwa makini kuangalia orodha hizo ili isitokee hata mtumishi mmoja akaachwa," anasema Kairuki.




COMMENTS

Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Watumishi wa umma sasa kupokea mishahara pamoja
Watumishi wa umma sasa kupokea mishahara pamoja
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5YW_AroiHbasPsTtk2am6l3WNWh3uoeK-serY2xw8wUqBEXlBADq3XLpxMAoOlYPXkeCvnlRStPC7jH02FJSLSkUBZ60MVy0loeIFW78AVqp-9CTfRdOyhLvnkaVTznDxAOobyeNzdS4/s400/C-fM1-kXsAIcPvG.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh5YW_AroiHbasPsTtk2am6l3WNWh3uoeK-serY2xw8wUqBEXlBADq3XLpxMAoOlYPXkeCvnlRStPC7jH02FJSLSkUBZ60MVy0loeIFW78AVqp-9CTfRdOyhLvnkaVTznDxAOobyeNzdS4/s72-c/C-fM1-kXsAIcPvG.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/watumishi-wa-umma-sasa-kupokea.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/watumishi-wa-umma-sasa-kupokea.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago