Sunday, August 06, 2017 Kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Kenya unaotarajiwa kufanyika Jumanne ya w...
Kampeni za kuwania urais katika uchaguzi mkuu nchini Kenya unaotarajiwa kufanyika Jumanne ya wiki ijayo, zimehitimishwa hapo jana kwa vinara wawili wanaopewa nafasi kubwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kuhitimisha kampeni zao kwa kuwataka wananchi kuwa watulivu na kudumisha amani.
Akifunga kampeni hizo kiongozi wa muungano wa Upinzani NASA Raila Odinga amewataka wapiga kura kujitokeza kwa wingi kumpigia kura na kuahidi kuwa akiingia madarakani ataondoa rushwa ambayo anasema mpinzani wake Uhuru Kenyatta ameshindwa kuiondoa.
Naye Mgombea wa Jubilee na rais wa sasa Uhuru Kenyatta ameahidi elimu bure kwa wakenya wote kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari na pia kukamilisha miradi ambayo tayari wameianza kama serikali.
Uchaguzi huo unaoangaziwa sana kutokana na mvutano wa kisiasa uliopo baina ya wagombea wawili wanaopewa nafasi kubwa unatarajia kuwa wa amani licha ya wasiwasi uliojitokeza kufuatia kifo cha mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Chriss Msando.