Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa amesema Ikulu haina taarifa kuhusu tuzo aliyoshinda Rais wa Jamhuri ya Mu...
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa amesema Ikulu haina
taarifa kuhusu tuzo aliyoshinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznia,
Dkt. John Magufuli nchini Ghana, kama Kiongozi Bora Barani Afrika.
Msigwa
ameeleza kwamba, inafahamika utaratibu wa tuzo yoyote lazima mtu
anayetunukiwa apewe taarifa rasmi, lakini mpaka sasa hawajapokea taarifa
yoyote kutoka kwa waandaaji wa tuzo hizo, hivyo hawajui lolote kama ni
kweli au la!
“Hatuna
taarifa ya tuzo hiyo, tunavyojua ni kwamba mtu yeyote anayetunukiwa
tuzo lazima apewe taarifa rasmi kutoka kwa watoaji, sasa hatujapata
taarifa yoyote mpaka sasa, nasikia ndio tuzo ambazo kina Monalisa
wameshinda, lakini hatujapokea taarifa rasmi kuhusu tuzo hiyo, hivyo
siwezi nikaizungumzia”, amesema Msigwa.
Tuzo
hiyo ambayo imetajwa kuwa ameshinda Rais Magufuli, imetolewa jana
Jumapili, Aprili 15, 2018 jijini Accra, Ghana, ambapo pia Watanzania
wengine katika tasnia ya filamu waliibuka washindi akiwemo Yvone Chery
‘Monalisa’ na Vincent Kigosi ‘Ray’.
chanzo; mpekuzi
chanzo; mpekuzi