post-feature-image
HomeHABARI

Monday, July 17, 2017 Igunga: Muuguzi Amchoma Binti Sindano ya Usingizi na Kisha Kumbaka

  17july2017 .     Muuguzi  anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Mgaya (26)...

Polisi Yaanza Kuchunguza Mlipuko Ulioteketeza Ofisi za Mawakili Fatma Karume na Lawrence Marsha
India: Mke aruhusiwa kuachwa na bwana kwa sababu nyumba yao haina choo
 

17july2017.

 
 
Muuguzi  anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Mgaya (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 mkazi wa kitongoji cha Mwagala B, Kijiji cha Mwagala.


Mtendaji wa Kata ya Igurubi, Ntemi James alisema uhalifu huo umefanyika Julai 14, mwaka huu saa 8 hadi alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama yake, Tatu Simbi ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya baada ya kushambuliwa kwa kipigo na mume wake. 


James alidai mtuhumiwa alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na ndipo alimpatia matibabu kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku akimchoma sindano ya usingizi ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa na usingizi.


Mtendaji huyo alidai kuwa muuguzi Damian alipoona mama wa binti huyo amelala, alimwambia waende wote chumba kingine ili akachukue dawa ya mama yake; lakini hata hivyo hakumpa dawa na badala yake alimwambia amchome sindano ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali sio mazuri. 


Baada ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano mbili na alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa sindano ya pili alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.


Alisema baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo alianza kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri na mwili wote. 


Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete alithibitisha kubakwa kwa binti huyo na muuguzi huyo na kueleza kuwa baada ya kupata taarifa hiyo, alituma timu ya wataalamu ambayo ilibaini binti huyo kubakwa na amelazwa kwenye kituo hicho na hali yake ni mbaya kwani hawezi kutembea.


Aidha, Dk Kalumbete alisema uchunguzi wa awali unaonesha binti huyo alichomwa sindano wakati alikuwa hata haumwi na hizo dawa nazo zimechangia kumsababishia kushindwa kutembea huku akiahidi kuwa baada ya uchunguzi, muuguzi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.


Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, John Mwaipopo alikiri kukamatwa kwa muuguzi baada ya kupokea taarifa ya kubakwa kwa binti huyo, alimwagiza Mkuu wa Polisi Igunga kumkamata muuguzi huyo Damian Mgaya ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.


Name

BURUDANI HABARI MAKALA MICHEZO
false
ltr
item
DIMBWI LA HABARI TZ: Monday, July 17, 2017 Igunga: Muuguzi Amchoma Binti Sindano ya Usingizi na Kisha Kumbaka
Monday, July 17, 2017 Igunga: Muuguzi Amchoma Binti Sindano ya Usingizi na Kisha Kumbaka
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYYl_IhAb_Z13G0Muj0WZNFpYj1c3SPfxzZ-3p_zLBG90-pFrJB1hsEveVIRTASRh-Mx21tNOML99RZNRviYZY403MLEX3ICgo7RnmEe7_met9ly_gpqN5E1uJveTs4xDXIRPPKozAp4b5/s400/dr.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhYYl_IhAb_Z13G0Muj0WZNFpYj1c3SPfxzZ-3p_zLBG90-pFrJB1hsEveVIRTASRh-Mx21tNOML99RZNRviYZY403MLEX3ICgo7RnmEe7_met9ly_gpqN5E1uJveTs4xDXIRPPKozAp4b5/s72-c/dr.jpg
DIMBWI LA HABARI TZ
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/monday-july-17-2017-igunga-muuguzi.html
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/
https://dimbwilahabari.blogspot.com/2017/07/monday-july-17-2017-igunga-muuguzi.html
true
8218800783604508792
UTF-8
Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago